Kuhusu FoniaAjira
FoniaAjira ni tovuti ya Kitanzania inayokusanya nafasi za kazi kutoka serikalini, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na kazi za ufundi — sehemu moja, kila siku.
Kila tangazo tunaloweka linaonyesha chanzo chake: tovuti ya mwajiri, tangazo la serikali, gazeti au mwajiri mwenyewe. Lengo ni moja: mtafuta kazi apate taarifa sahihi mapema, bila kulipa chochote.
Tunavyohakiki matangazo
- Matangazo ya waajiri yanapitiwa na timu yetu kabla ya kuonekana.
- Tangazo linaloomba pesa kutoka kwa mwombaji linaondolewa mara moja.
- Nafasi zinazopita tarehe ya mwisho zinafungwa zenyewe.
Wasiliana nasi
Email: josephahazi@gmail.com
Simu: 0683369779
WhatsApp: jiunge na channel
Faragha
Tunahifadhi taarifa ulizotupa (jina, email, simu, CV) ili kukusaidia kutafuta kazi tu. CV yako inaonekana kwa mwajiri pale unapomtumia maombi. Hatuuzi taarifa zako. Unaweza kuomba akaunti yako ifutwe muda wowote kwa kutuandikia.